1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ujerumani kujitanua zaidi n'gambo ?

29 Agosti 2006

Kujitanua zaidi Afghanistan kwa Bundeswehr,kunajadiliwa motomoto na kuchambuliwa na safu za wahariri wa magazeti ya ujerumani sawa na amri ya kutaka makampuni binafsi kushiriki katika biashara ya Lotto-bahati nasibu.

https://p.dw.com/p/CHV6

Idara ya Ujerumani inayosimamia mashindano sawa katika sekta ya biashara na kuzuwia kuoneana,imeitisha pawepo mashindano zaidi kati ya vituo vya bahati-nasibu humu nchini-maarufu “Lotto”.Kuanzia sasa, makampuni 16 ya kiserikali yanayoendesha bahati nasibu, hayataruhusiwa tena kugawana miongoni mwao kimkoa soko la kuendesha bahati nasibu.

Yametakiwa kuruhusu pia vituo vya kibinafsi kuchezesha bahati nasibu. Mada nyengine ni matumizi ya Bundeswehr-jeshi la Ujerumani nchi za n’gambo kama vile Afghanistan na Kongo:

Tukianza na mada ya kushirikishwa zaidi vikosi vya Ujerumani nchi za nje kuhifadhi amani, waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung amekanusha taarifa za vyombo vya habari kuwa wanajeshi wa ujerumani watapelekwa hata kusini mwa Afghanistan kuliko chacha machafuko.

Gazeti la MITTLEBAYERISCHE ZEITUNG kutoka Regensburg linaona kwqamba kabla mtu kujitosa zaidi hatarini,anapaswa kujiuliza maswali ya busara:Kujitawanya kila pembe ya dunia kwa vikosi vya ujerumani kulinda amani kuna maana au la ? Je, tunapaswa nchini afghanistna bunduki mkononi kuthibitisha kwamba sisi ni hirimu moja na dola kama Uingereza au Spain ? Je, kujiingiza katika balaa la siasa za Kongo,kunastahiki hatari zake ?

Kutokana na historia yao wajerumani ni barabara kujitwika dhamana ya kulinda amani karibu na mpaka na Israel ? Ujerumani kutojiingiza kijeshi nchi za n’gambo ,daima kumekuwa siasa yake ya miongo kadhaa iliopita.Iikuaje leo hatuthubutu kusema., la,hatutaki kuingizwa ?-lauliza Mittlebayerische Zeitung.

Ama katika gazeti la Kurier linalotoka Wiesbaden tunasoma:

„Uwezekano wa kutakiwa Ujerumani kuchangia vikosi zaidi nchini Afghanistan kutaongoza kufunuwa kawa zaidi la makosa yanayofanywa na serikali mjini Berlin:

Kujiunga na Ujerumani na vikosi vya ISAF huko, Bunge la Ujerumani-Bundestag- lilitoa idhini ya kutosha .Sasa kupanua jukumu hilo hakuhitaji idhini mpya ya Bunge hilo.Na huu ni mtindo unatia wasi wasi na shaka shaka.Kwani, mara tu jeshi la Ujerumani laweza kujikuta limejitosa vitani.

Wakosoaji walikwishaonya juu ya uwezekano huu. Ni maoni ya KURIER kutoka Wiesbaden.

Ama GENERAL-ANZEIGER kutoka mjini Reutlinge, laandika kwamba, wanasiasa juu ya hivyo hawahisi uzuri.

Katiba ya Ujerumani inaruhusu katika swali la ulinzi na la ushirika wa kiulinzi majeshi ya ujerumani kuweza kutumika,lakini kuilinda nchi kwa maana hasa iliokusudiwa,hakuna maana kujitumbukiza katika kila balaa linalozuka nchi za nje….

Likitukamilishia mada hii, FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG laandika kuwa juu ya hivyo, maombi kwa Ujerumani na kwa Bundeswehr kujitawanya zaidi nchini Afghanistan yatazidi kuwa wazi kila hali huko ikizidi kuchafuka.Kwani hakuna anaetaka kuwatia dosari wanajeshi wa Ujerumani kuwa waoga wanakimbia….

Gazeti lamaliza:

„Ikiwa Afghanistan,Kongo au Lebanon,wanajeshi hawapelekwi huko kujenga shule au kusimamia uchaguzi.Watu wanapaswa kuelewa kuwa huko kila siku wanakabiliwa na uwezekano wa kuzuka mapigano.“

Tukija sasa katika amri iliotolewa na Idara ya kusimamia usawa wa mashindano ya kibiashara-Bundeskartellamt- gazeti la NEUE RUHR/NEUE RHEIN-ZEITUNG kutoka Essen laandika:

„Idara hii ya kusimamia ushindani wa kibiashara imeleeza kile ambacho kila mmoja akikijua:

Wanasiasa hawashughulishwi hapa na kupambana na tabia ya kucheza kamari au bahati nasibu iliowavaa raia wake ,bali kinacho washughulisha ni mapato kutoka kamari hizo.Euro bilioni 5 serikali za mikoa kila zinachota kila mwaka kutoka mfereji wa bahati-nasibu za Lotto.“