Jeshi la Sri Lanka lashambulia waasi wa Tamil | Habari za Ulimwengu | DW | 21.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Jeshi la Sri Lanka lashambulia waasi wa Tamil

COLOMBO:

Nchini sri Lanka ,vikosi vya serikali vimeshambulia ngome za waasi wa tamila Tigers kwenye maeneo ya mstari wa mbele wa mapambano katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.Wizara ya Ulinzi imesema kuwa shambulio hilo liliwasha moto wa mapigano makali ambayo yamesababisha waasi 29 na askari wawili wa serikali kuuawa.

Mapigano ya sasa yamekuja baada ya Sri Lanka kuufuta rasmi mkataba na waasi wa kutohujumiana ambao umekuwa ukiheshimiwa kwa kiasia kwa miaka inayokaribia 6. serikali inawalaumu waasi hao kwa kutumia mkataba uliochochewa na Oslo kujilimbikizia silaha na pia kushambulia viuo vya kijeshi vy a serikali pamoja na kuwahujumu raia. Watu maia kwa maelfu wameuawa tangu waasi waKitamil waanzishe kampeini ya kutaka kujitenga mwaka wa 1972.Wanataka waTamil wachache wajitawale wakipewa maeneo ya kusini na mashariki mwa kisiwa hicho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com