1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la NATO lashambulia Tripoli

8 Juni 2011

Ndege za kivita za NATO zimeushambulia mji wa Tripoli, mashambulizi makali zaidi kufanywa kwenye mji huo tangu Umoja wa Mataifa ulipopitisha azimio la kuweka marufuku ya ndege kuruka kwenye anga ya Libya, mwezi Machi.

https://p.dw.com/p/11Whi
Moja ya ndege za NATOPicha: Picture-Alliance/dpa

Akizungumza jana kwa njia ya redio wakati wa mashambulio hayo kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi aliahidi kuendelea kupambana. Msemaji wa serikali ya Libya, Mussa Ibrahim amesema watu 31 wameuawa wakati wa mashambulio yapatayo 60 yaliyofanywa na NATO.

Miripuko kadhaa ilisikika kuzunguka eneo la Kanali Gaddafi. Waandishi wa habari walionyeshwa maiti moja. Leo, mawaziri wa ulinzi wa NATO wanatarajia kukutana mjini Brussels kutathmini kampeni yao nchini Libya. Mtoto wa kike wa Kanali Gaddafi, Aisha amefungua mashtaka ya uhalifu wa kivita dhidi ya NATO katika mahakama ya Ubelgiji.

Mashtaka hayo yanahusishwa na mashambulio yaliyofanywa Aprili 30 mwaka huu, ambayo kwa mujibu wa maafisa wa Libya, wanafamilia wanne wa Gaddafi waliuawa. Waasi kwenye mji wa pili kwa ukubwa wa Benghazi wametembelewa na mjumbe wa ngazi ya juu wa Urusi. Na katika Umoja wa Mataifa, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa, Alain Juppe amesema mpango wa kusimamisha mapigano nchini Libya utajadiliwa kesho huko Abu Dhabi.

Mikhail Marglov Benghazi Libyen
Mikhail Marglov, Mjumbe maalum wa rais wa Urusi katika masuala ya AfrikaPicha: dapd