1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Libya lakaribia kuitwaa Sirte

Caro Robi
23 Novemba 2016

Majeshi ya Libya yanasema yanaikaribia ngome ya mwisho wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) katika mji wa Sirte, ikiwa ni kampeni ya kuwang'oa kabisa nchini humo.

https://p.dw.com/p/2T6lB
Lybien Armee und UN-Truppen patrouillieren nach einem Gefecht mit dem IS
Picha: Reuters/H. Amara

Muda mfupi kabla ya kuanza kwa opresheni hiyo ya kuukomboa mji wa Sirte hapo jana (Novemba 22), vidio iliyoonekana katika mitandao ilionyesha wapiganaji wakitumia vipaza sauti kuwahimiza wanawake na watoto kuondoka eneo hilo na kuwaahidi usalama wao wanapoondoka.

Vikiungwa mkono na mashambulizi ya angani ya Marekani, vikosi vya majeshi yanayounga mkono serikali ya Líbya yamekuwa yakipiga hatua dhidi ya wanamgambo wa IS walioko katika eneo hilo lililo karibu na Bahari ya Meditarrania.

IS iliudhibiti mji huo mwaka jana na iwapo jeshi na wapiganaji watiifu kwa serikali watafanikiwa kuukomboa, basi IS itapoteza ngome yake pekee nchini Libya.

Operesheni ya kuukomboa mji huo ilianza tangu mwezi Mei 2016.