1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ethiopia linasonga mbele mji mkuu wa Tigray

Saumu Mwasimba
24 Novemba 2020

Jeshi la serikali ya Ethiopia limesema liko umbali wa kilomita 60 kuufikia mji mkuu wa Tigray Mekele.

https://p.dw.com/p/3lkTA
Äthiopien | Videostill Ethiopian News Agency | Militär
Picha: Ethiopian News Agency/AP Photo/picture alliance

Kwa upande mwingine msemaji wa vikosi vya kundi la TPLF vinavyopambana na jeshi hilo la Ethiopia amesema jeshi lao limeharibu kabisa kitengo cha magari ya silaha ya jeshi la serikali. Getachew Reda, msemaji wa jeshi la Tigray ametangaza leo jumanne kwamba wameharibu kabisa kitengo cha silaha cha jeshi la Ethiopia huku kiongozi wa kundi hilo la TPLF Debretsion Gebremichael akisema kwamba waziri mkuu Abiy anajaribu kufunika ukweli juu ya kushambuliwa kwa jeshi lake na vikosi vya Tigray.

Gebremichael amesema vitisho vilitotolewa na Abiy dhidi ya Tigray ni mbinu ya kuvuta mda kutokana na kipigo walichokipata wanajeshi wake. Kupitia shirika la habari la AFP kiongozi huyo wa Tigray amesema Abiy haelewi Watigray ni kina nani. Amejinadi kiongozi huyo kwamba wao ni watu wenye misimamo na wako tayari kufa kulinda haki zao kusimamia jimbo lao.

Mawasiliano duni na kiasi ya watu 40,000 wameyakimbia makazi yao kutokana na machafuko

Äthiopien Tigray Konflikt Flüchtlinge
Baadhi ya wakazi wanaokimbia vita eneo la TigrayPicha: Mohamed Nureldin Abdallah/Reuters

Msemaji wa serikali ya Ethiopia hakupatikana kutoa tamko kuhusiana na madai ya Tigrai. Hata hivyo shirika la habari la Reuters limesema haliwezi kuthibitisha taarifa zote zilizotolewa na pande zote mbili kutokana na kukatwa kwa mawasiliana ya simu na mtandao katika eneo la Tigray.Mamia ya watu wameuwawa tangu Novemba 4 ulipozuka mgogoro huu na kiasi 40,000 wengine wameikimbilia Sudan. Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephanie Dujarric akizungumza kuhusiana na hali ilivyo kwa sasa amesema.

Kufuatia hali ilivyo Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujaric, amesikia akisema ''Bado tuna wasiwasi mkubwa na usalama wa raia katika jimbo la Tigray na hasa watu zaidi ya nusu milioni ikiwemo wafanyakazi wa mashirika ya msaada 200 waliobakia Mekelle,kufuatia taarifa kwamba mapigano huenda yakaingia katika mji huo ndani ya saa kadhaa zijazo.''

Miji kadhaa imedhibitiwa na jeshi la Ethiopia kuelekea mji mkuu wa Tigray uitwao Mekele

Mkuu wa jeshi la Ethiopia Brigadier jenerali Tesfaye Ayalew, amesema tayari wameikamata miji ya kuelekea kaskazini na kusini na wako umbali wa maili 37 kuufikia mji huo wa Mekele,mji mkuu wa Tigray ambako ndiko yaliko makaazi ya TPLF.

Soma zaidi:Abiy Ahmed: Vikosi vya Tigray vijisalimishe ndani ya masaa 72

Jana Waziri Mkuu Abiy Ahmed alitowa muda wa saa 72 wa kujisalimisha kwa viongozi wa TPLF lakini kiongozi wao amesema wako tayari kufa katika mapambano ya kuulinda kile wanachokiita haki yao. Marekani pia Jumatatu ilitowa mwito wa kufanyika mazungumzo kati ya pande hizo mbili na kuziunga mkono juhudi zinazoongozwa na rais wa Afrija Kusini Cyril Ramaphosa na Umoja wa Afrika kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu.

Vyanzo: AFP/RTR