1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Chad laua mamia ya waasi

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTXb

Jeshi la Chad limeripoti kwamba limewaua mamia ya waasi kwenye mapigano makali mashariki mwa nchi hiyo. Mapigano hayo yalizuka baada ya makundi mawili ya waasi kumaliza usitishwaji wa mapigano mwishoni mwa juma lililopita uliodumu mwezi mmoja. Msemaji wa kundi la waasi la UFDD analilaumu jeshi la Chad kwa kuanzisha mashambulizi hayo. Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Ulaya kinatarajiwa kupelekwa katika eneo hilo kuanzia mwanzoni mwa mwaka ujao kulinda juhudi za utoaji wa huduma za kiutu kwa wakimbizi takriban laki nne walioyakimbia machafuko nchini Sudan na Chad.