JERUSALEM:Waziri Steinmeir aitaka Israel kuendelea na juhudi za amani | Habari za Ulimwengu | DW | 07.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM:Waziri Steinmeir aitaka Israel kuendelea na juhudi za amani

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir ameitaka Israel kuendelea na juhudi za kutafuta amani na wapalestina.

Katika mkutano wake huko Jerusalem na waziri wa mambo ya nje wa Israel Tzipi Livni, Steinmeir amesema kuendelea kwa juhudi hizo za amani mashariki ya Kati kutabakia kuwa suala muhimu katika sera za nje za Umoja wa Ulaya. Livni kwa upande wake amesema anapanga kwenda mjini Cairo baadae wiki hii kujadili juu ya kufufua mpango wa amani uliopendekezwa na nchi za kiarabu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com