1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Wabunge waidhinisha ombi la rais Katsav

26 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXq

Bunge la Israel limekubali ombi la rais Moshe Katsav la kutaka kuondoka kazini kwa muda kwa sababu ya madai ya ubakaji na matumizi mabaya ya madaraka.Wabunge walipiga kura 13 kwa 11 kukubali ombi la kuchukua livu ya miezi mitatu,ambayo pia inaweza kurefushwa hadi miezi sita.Siku ya Jumatano kwenye mkutano na waandishi wa habari, rais Katsav kwa hamaki alikanusha shutuma za ubakaji na alisema atajiondosha kwa muda kutoka wadhifa huo usio kuwa na uzito,lakini hatojiuzulu.Kwa upande mwingine,waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema kwa hali ilivyo,rais Moshe Katsav hana budi ila kuondoka madarakani. Kura ya maoni inaonyesha kuwa raia wengi wa Israel wanamtaka Katsav ajiuzulu kwa sababu ya kashfa hiyo.