JERUSALEM:Tzipi Livni akutana na waziri mkuu Salam Fayad wa Palestina | Habari za Ulimwengu | DW | 09.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM:Tzipi Livni akutana na waziri mkuu Salam Fayad wa Palestina

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Tzipi Livni amekutana na waziri mkuu wa Palestina Salam Fayad kwa mara ya kwanza tangu kuundwa kwa serikali mpya ya mamlaka ya wapalestina.

Kwa mujibu wa afisi ya waziri wa mambo ya nje wa Israel,viongozi hao wawili walijadili juu ya jinsi mataifa ya kirabu yatakavyoweza kuunga mkono mpango wa kisiasa katika eneo hilo.

Hapo jana serikali ya Israel iliidhinisha kutolewa kwa wafungwa 250 wakipalestina kufuatia ahadi aliyoitoa waziri mkuu Ehud Olmert kwa rais Mahmoud Abbas katika mkutano uliofanyika mnamo mwezi juni.

Wakati huo huo wanajeshi wa Israel wamemuua kwa kumpiga risasi mwanachama wa kundi la Islamic Jihad katika eneo la kaskazini mwa ukingo wa magharibi kwenye mji wa Jenin..

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com