JERUSALEM:Olmert kuwekwa katika kitimoto juu ya vita vya Lebanon mwaka jana | Habari za Ulimwengu | DW | 29.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM:Olmert kuwekwa katika kitimoto juu ya vita vya Lebanon mwaka jana

Waziri Mkuu wa Isreal bwana Ehud Olmert amesema kuwa hana nia ya kujiuzulu kutokana na lawama juu ya jinsi serikali yake ilivyoendesha vita vya nchini Lebanon mwaka jana.

Msemaji wa waziri mkuu huyo ameeleza hayo kabla ya kuchapishwa hapo kesho, ripoti juu ya makosa yaliyotendeka katika kuongoza vita hivyo.

Ripoti hiyo inatarijiwa kushutumu hatua za pupa zilizochukuliwa na serikali ya waziri mkuu Olmert baada ya wapiganaji wa Hezbollah kufanya mashambulio na kuwateka nyara askari wawili wa Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com