1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Ehud Olmert akabiliwa na wakati mgumu

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC58

Shinikizo za kumtaka waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ajiuzulu zimeongezeka.

Bwana Olmert leo alikabiliwa na wakati mgumu bungeni huku kukiwa na maandamano ya kumpinga waziri mkuu huyo katika bara bara za mji wa Jerusalem.

Bunge la Knesset kwa sasa linaijadili ripoti ya tume ya Winograd iliyotolewa siku ya jumatatu kuhusu jinsi waziri mkuu Ehud Olmert alivyo wajibika katika vita vya Lebanon vya mwaka uliopita.

Hadi sasa bwana Olmert amepuuza mwito unaomtaka ajiuzulu licha ya wanachama wenye uwezo mkubwa katika chama cha Kadima kama waziri wa mambo ya nje bibi Tzippi Livni kumtaka ajiuzulu.

Maelfu ya watu wanatarajiwa kuandamana katika mji wa Tel Aviv kumpinga waziri mkuu Ehud Olmert.

Ripoti hiyo imemlaumu bwana Olmert kwa kushindwa vibaya katika vita dhidi ya wananmgambo wa Hezbollah nchini Lebanon imesema Olmert aliharakisha na wala hakutumia busara kabla ya kuanzisha vita hivyo.