JERUSALEM:BibI Rice amekutana na rais Mahmoud Abbas | Habari za Ulimwengu | DW | 15.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM:BibI Rice amekutana na rais Mahmoud Abbas

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice amekutana na kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas akiwa katika ziara ya siku nne mashariki ya kati.

Ziara hiyo inakusudia kuweka msingi wa mkutano wa amani kati ya Israel na Palestina unaodhaminiwa na Marekani uliopangiwa kufanyika mwezi ujao wa Novemba.

Bibi Rice ametahadharisha kuwa ziara yake hii isitegemewe kuleta suluhisho.

Rais Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert wote wamesema kuwa wanatarajia kuwa mkutano wa mwezi Novemba utakuwa chanzo cha majadiliano kuhusu kupatikana taifa la Palestina.

Matatizo hayo yanakabiliwa na utata juu ya mipaka ya taifa jipya la Palestina, mustakabali wa mji mtakatifu wa Jerusalem na hatima ya mamilioni ya wakimbizi wa Kipalestina.

Bibi Rice pia anatarajiwa kuzitemebelea Misri na Jordan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com