1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Abbas na Olmert wamaliza mazungmzo

16 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBi1

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na Kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas wamefanya mazungumzo kuhusu mipango ya kuusaidia utawala wa rais Mahmoud Abbas katika ukingo wa magharibi.

Israel imehakikisha kuwa itawaachia huru wafungwa 250 wa kipalestina katika hatua ya kutaka kufufua upya mazungumzo ya amani. Pia Israel ilitangaza jana kuwa haitawalenga tena wapiganaji 180 wa kundi la Fatah ikiwa watasimaisha mashambulio yao dhidi ya taifa la Kiyahudi.

Marekani imemtaka bwana Olmert aanze tena mazungumzo ya amani na rais Mahmoud Abbas baada ya kundi la Hamas kutwaa mamlaka kwa nguvu katika ukanda wa Gaza mwezi uliopita.

Mwishoni mwa wiki rais Abbas alitangaza baraza lake jipya la mawaziri kuchukuwa mahala pa baraza la zamani la chama cha Hamas kilichoshinda uchaguzi wa mwaka 2006.