1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Watu watatu wauwawa kwenye shambulio la bomu

29 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWp

Watu watatu wameuwawa kufuatia shambulio la bomu lililofanyw na mtu wa kujitoa muhanga maisha kwenye mji wa mapumziko wa Eilat nchini Israel ulio katika bahari ya Shamu.

Shambulio hilo ni la kwanza dhidi ya Israel katika kipindi cha miezi tisa. Shambulio la mwisho lilifanywa nchini Israel mnamo tarehe 17 mwezi Aprili mwaka jana mjini Tel Aviv.