1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Wapalestina wawili wauwawa

Wanajeshi wa Israel leo wamemuua mwanamgambo wa kundi la Hamas wakati wa operesheni ya jeshi iliyofanywa kusini mwa Ukanda wa Gaza. Maafisa wa Hamas na wa hospitali wamethibithisha taarifa hiyo.

Katika tukio lengine huko Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan vikosi vya Israel vimefanya uvamizi na kumjeruhi vibaya mpalestina mmoja aliyejaribu kumdunga kisu mwanajeshi wa Israel. Famila ya mpalestina huyo imesema amekufa muda mfupi baadaye kufuatia majeraha aliyoyapata.

Kundi la Hamas mjini Gaza limesema mpiganaji wake huyo alikuwa akijaribu kukabiliana na kifaru cha Israel karibu na mji wa Al Fukhari, mashariki mwa Khan Younis, wakati aliposhambuliwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com