1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Shimon Peres kuwania urais wa Israel

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwY

Naibu waziri mkuu wa Israel, Shimon Peres, ametangaza hii leo kwamba atagombea wadhifa wa urais katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 13 mwezi ujao nchini Israel.

Rais wa Israel, Moshe Katsav, anayesisitiza hakufanya makosa kuhusiana na kashfa ya ubakaji na uhusiano wa kimapenzi uliokiuka sheria, alijiondoa kwa muda mapema mwaka huu ili kukabiliana na mashataka yanayomkabili, lakini akasita kujiuzulu.

Hakuna mashtaka rasmi yaliyowasilishwa mahakamani dhidi ya rais Katsav kufikia sasa, lakini mwanasheria mkuu wa Israel, jenerali Meni Mazuz, ameashiria mpango wake wa kufanya hivyo.

Awamu ya rais Perez inamalizika mwishoni mwa msimu huu wa kiangazi.

Shimon Peres mwenye umri wa miaka 83, ameidhinishwa na chama chake cha Kadima. Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ameahidi kumuunga mkono Shimon Peres akisema anafaa kuwa rais wa Israel.