JERUSALEM: Shimon asema Israel ipo tayari kufanya mazungumzo na Syria | Habari za Ulimwengu | DW | 11.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Shimon asema Israel ipo tayari kufanya mazungumzo na Syria

Naibu waziri Mkuu wa Israel bwana Shimon Peres amesema kuwa rais Bashar al Assad wa Syria anakaribishwa nchini Israel kwa ajili ya mazungumzo juu ya kuleta amani.

Bwana Peres amesema hayo kujibu kauli iliyotolewa na rais Assad wa Syria kwamba yupo tayari kufanya mazungumzo na Israel.

Bwana Peres ameeleza kuwa Israel itakuwa tayari kufanya mazungumzo, ikiwa Syria inataka kufanya hivyo, lakini waziri Mkuu wa Israel bwana Ehud Olmert amejiweka kando na mwaliko huo.

Mazungumzo ya amani baina ya Syria na Israel yalivunjika miaka sita iliyopita baada ya Syria kuitaka Israel irejeshe milima ya Golan ambayo imekuwa inaikalia tokea vita vya mwaka wa 1967.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com