1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Rais Moshe Katsav karibu kufunguliwa mashtaka ya ubakaji

18 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1k

Wendeshamashtaka mjini Jerusalem wameanza kuandaa kielelezo cha kumfungulia mashtaka rais wa Israeli, Moshe Katsav, kufuatia madai ya polisi kwamba imekusanya ushahidi kwamba rais Katsav alihusika katika vitendo vya ubakaji wa wafanyakazi wa ofisi yake. Vyombo vya habari nchini Israeli, vimesema inaelekea mwanasheria mkuu wa jamhuri atachukuwa hatua ya kumfungulia mashtaka mnamo muda wa wiki mbili. Waziri wa sheria imejizuwia kuzungumzia lolote juu ya suala hilo. Rais, Moshe Katsav, mwenye umri wa miaka 60, alikana madai hayo ya polisi na kusema hiyo ni hukumu bila sheria. Wakili wake amesema huenda rais Katsav kajiuzulu ikiwa atafunguliwa mashtaka.