1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Olmert kufanyiwa upasuaji wa sarakani

29 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BX

Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert ametangaza kuwa ana sarakani ya tezi la kibofu cha mkojo.Katika mkutano wa ghafula pamoja na waandishi wa habari mjini Jerusalem,Olmert alisema,sarakani hiyo ni changa na anataraji kuwa na upasuaji mdogo. Akaongezea,madaktari wamemuarifu kuwa ugonjwa huo hautoathiri uwezo wake wa kufanya kazi.