JERUSALEM : Mjadala juu ya Rais Katsav waanza | Habari za Ulimwengu | DW | 15.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM : Mjadala juu ya Rais Katsav waanza

Wabunge wa Israel wameanza mjadala juu ya iwapo kumshtaki Rais Moshe Katsav ambaye amechukuwa likizo ya bila ya malipo kutokana na kukabiliwa na madai ya ubakaji.

Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali nchini Israel alimuarifu Katsav mwezi uliopita kwamba yumkini akamshtaki kwa madai ya ubakaji, shambulio la ngono na kutumia vibaya madaraka yake.Hata hivyo Rais huyo mwenye umri wa miaka 61 anastahiki kusikilizwa kwenye kikao rasmi kabla ya mwendesha mashtaka huyo wa serikali kutowa uamuzi wa mwisho.

Katsav amekanusha kufanya kosa lolote lile na amekataa wito wa kumtaka ajiuzulu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com