JERUSALEM: Marekani kuimarisha msaada wa kijeshi Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 29.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Marekani kuimarisha msaada wa kijeshi Israel

Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert amethibitisha kuwa Marekani inapanga kuipatia Israel msaada zaidi wa kijeshi.Aliwaambia waandishi wa habari kwenye mkutano wake wa kila juma pamoja na baraza la mawaziri kuwa Washington imekubali kuongeza msaada huo kwa asilimia 25.Hiyo ikiwa ni zaidi ya Dola bilioni 30 katika kipindi cha miaka kumi ijayo.

Tangazo hilo linafuatia ripoti iliyosema kuwa Marekani inatayarisha mikataba kadhaa ya kijeshi. Azma ya mikataba hiyo ni kuziimarisha kijeshi Saudi Arabia na washirika wengine wa Marekani katika Mashariki ya Kati.

Hatua hiyo inatazamwa kama jitahada za kupambana na ushawishi wa Iran unaozidi kutia mizizi katika kanda hiyo ya Ghuba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com