1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Kazi za ukarabati zaendelea karibu na Msikiti wa Al-Aqsa

11 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCT8

Licha ya upinzani mkali,Israel imeendelea na kazi za ukarabati kwenye eneo la Msikiti wa Al-Aqsa. Wajenzi,chini ya ulinzi wa polisi wapato 2,000 walirejea kuendelea na kazi za ukarabati kwenye daraja linalotumiwa na watu wanaokwenda kwa miguu.Polisi wamesema,ili kuzuia mapambano mapya, Wapalestina chini ya umri wa miaka 45 hawaruhusiwi kwenda eneo hilo.Tangu siku kadhaa, Wapalestina wanaandamana wakisema kuwa kazi za ukarabati huenda zikahatarisha msingi wa Msikiti wa Al-Aqsa.