1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel yasema itaonyesha uvumilivu na subira

26 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCp7

Waziri mkuu wa Israel,Ehud Olmert amesema Israel itaonyesha kile alichokiita „uvumilivu na subira“ kuhusu mashambulio ya makombora yaliofanywa na Wapalestina saa chache tu baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuanza kufanya kazi.Tawi la kijeshi la Hamas limesema Israel ilirushiwa makombora hayo kutoka Gaza kwa sababu vikosi vyake bado vipo katika ardhi ya Gaza.Kundi la Islamic Jihad pia limedai kuwa lilihusika na mashambulio hayo,likisema litakubali kuweka chini silaha ikiwa vikosi vya Kiisraeli vitaondoka Ukingo wa Magharibi.Kuambatana na makubaliano ya kusitisha mashambulio,makundi ya wanamgambo wa Kipalestina yasite kuirushia Israel makombora na Israel nayo iondoke Gaza.Msemaji wa serikali ya Wapalestina inayoongozwa na Hamas,amelaani mashambulio yaliofanywa na amesema,makundi yote yanapaswa kuheshimu makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyoanza kufanya kazi mapema leo hii.