JERUSALEM: Israel yaonya kuchukua hatua kali zaidi
20 Mei 2007Matangazo
Waziri mkuu wa Israel,Ehud Olmert ametishia kuchukua hatua kali zaidi za kijeshi katika Ukanda wa Gaza ikiwa kundi la Hamas halitoacha
kurusha makombora kusini mwa Israel.Mashambulio ya angani ya Israel hii leo yameua Wapalestina 3 walioshukiwa kuwa wanamgambo wa Hamas.Kama Wapalestina 21 wameua katika mashambulio ya siku tano yaliofanywa na ndege na vifaru vya Israel.