1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel yaifunga mipaka ya maeneo ya Wapalestina

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCND

Jeshi la Israel limeyafunga maeneo ya Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan mpaka Jumatatu jioni wiki ijayo.

Hatua hiyo ya kuyafungwa maeneo hayo ya Wapalestina imechukuliwa kwa sababu ya hofu ya kufanywa mashambulio wakati wa sherehe ya kiyahudi ya Purim.

Uamuzi huo ulioanza kutekelezwa saa sita usiku wa kuamkia leo, ulichukuliwa na waziri wa ulinzi wa Israel, Amir Peretz, baada ya kutathimini hali ya usalama katika maeneo hayo ya Wapalestina. Sherehe ya Purim ambayo hufanyika Jumapili na Jumatatu, inajumulisha maandamano mfano wa kanivali na kuvaa mavazi ya fensi.

Hapo awali jeshi la Israel lilimaliza operesheni yake ya siku tano ya kuuzingira mji wa Nablus katika Ukingo wa magharibi wa mto Jordan. Ufyatulianaji wa risasi umeripotiwa karibu na msikiti mmoja mjini Nablus.