1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Israel na Palestina wakutana.

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkY

Kwa mara ya kwanza katika historia yake , jumuiya ya nchi za Kiarabu itatuma ujumbe nchini Israel wiki hii , ili kujadili hatua za kuleta amani pamoja na kitisho kinacholetwa na kundi la Hamas pamoja na makundi mengine ya Kiislamu yenye imani kali.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya kigeni wa Israel Tzipi Livni amekutana na waziri mkuu wa Palestina Salam Fayyad kwa mara ya kwanza tangu kiongozi huyo wa Palestina kuchukua madaraka.

Ofisi ya Livni imesema kuwa viongozi hao wawili walijadili njia ambapo mataifa ya Kiarabu yanaweza kuunga mkono hatua za kisiasa katika eneo hilo.

Hapo mapema , jana Jumapili baraza la mawaziri liliidhinisha kuachiliwa kwa wafungwa 250 wa Kipalestina , kufuatia ahadi iliyotolewa na waziri mkuu Ehud Olmert kwa rais Mahmoud Abbas katika mkutano mwezi wa Juni. Wakati huo huo katika mji wa kaskazini ulioko katika eneo la Ukingo wa magharibi wa Jenin , majeshi ya Israel yamempiga risasi na kumuua mwanaharakati mmoja wa Kipalestina.