1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Israel kuachilia wafungwa 250 wa Kipalestina

8 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkp

Baraza la mawaziri la Israel leo limekubali kuachiliwa kwa wafungwa 250 wa Kipalestina katika jitihada kadhaa za hivi karibuni za kumpa nguvu Rais Mahmoud Abbas wa Palestina anayeungwa mkono na mataifa ya magharibi kufuatia kundi la Hamas kuutwaa Ukanda wa Gaza.

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert ameliambia baraza lake la mawaziri kwamba anafikiri hiyo ni hatua inayostahiki kuchukuliwa kwa sababu wanataka kutumia kila njia ambazo zinaweza kuwapa nguvu watu wa msimamo wa wastani katika Mamlaka ya Palestina.

Olmert ameahidi kuwaachilia huru wafungwa hao wa kundi la Fatah la Rais Abbas katika mkutano na kiongozi huyo wa Palestina hapo tarehe 25 mwezi wa Juni ikiwa ni sehemu ya kampeni ya mataifa ya magharibi kuimarisha serikali mpya ambayo ameitangaza baada ya kuitimuwa serikali ya umoja wa kitaifa aliyoiunda na kundi la siasa kali za Kiislam la Hamas.