1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERICHO:Waziri Mkuu wa Israel aenda kwa wapalestina kwa mara ya kwanza

7 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbP

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na Rais wa mamlaka ya wapalestina, Mahamoud Abbas wamekuwa na mazungumzo katika mji wa ukingo wa magharibi wa Jerico.

Hii ni mara ya kwanza kwa Waziri Mkuu wa Israel kutembelea maeneo ya wapalestina katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

Olmert alisema kuwa ana matumaini ya kuanza tena kwa majadiliano ya kuelekea kuanzishwa kwa taifa la Palestina haraka iwezekanavyo.

Hata hivyo maafisa wa Israel walikuwa makini kuzungumzia iwapo mkutano wa wakuu hao si kilele cha muafaka wa masuala kama ya mpaka na majaaliwa ya mji wa Jerusalem pamoja na wakimbizi wa Kipalestina.