1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je Waislamu wenye imani kali wataweza kuikomboa meli ya mafuta ya Saudia?

Sekione Kitojo24 Novemba 2008

Mazungumzo bado yanaendelea katika juhudi za kuikomboa meli ya mafuta ya Saudi Arabia iliyotekwa nyara siku nane zilizopita na maharamia.

https://p.dw.com/p/G0rX
Meli ya kivita ya India INS Tabar kulia ikisindikiza meli ya MV Jag Arnav kwenda katika eneo salama baada ya kuiokoa kutokana na jaribio la maharamia wa kisomali kutaka kuiteka nyara.Picha: AP

Mazungumzo ya kuiacha huru meli ya mafuta ya Saudi Arabia iliyotekwa nyara na maharamia yanaendelea. Meli hiyo ilitekwa nyara siku nane zilizopita katika pwani ya Kenya. Kwa kuiteka nyara meli ambayo inamilikiwa na taifa la kiarabu maharamia kwa mara ya kwanza wanakumbana na upinzani kutoka kwa wanamgambo wa Kiislamu , ambao wanapigana nchini Somalia kuwania udhibiti wa nchi hiyo na katika miezi iliyopita wameweza kukamata baadhi ya miji katika taifa hilo la pembe ya Afrika.


Kampuni la mafuta nchini Saudi Arabia la Aramco liko wakati wote katika mbinyo. Hadi Novemba 30 linapaswa kulipa kiasi cha dola milioni 25 ili kuikomboa meli hiyo, la sivyo wanatishia maharamia hao kama wanavyosema , kufanya uharibifu mkubwa.

Hapa sio tu kwamba kundi zima la wafanyakazi wa meli hiyo maisha yao yako hatarini, lakini pia mafuta yasiyosafishwa yenye thamani ya dollar milioni 100, pamoja na uwezekano wa uchafuzi mkubwa kabisa wa mazingira.

Iwapo maharamia hao watatekeleza azma yao, wakayamwaga mafuta hayo baharini , maafa yatakayotokea kwa mwamba wa matumbawe katika bahari ya Sham na sehemu ya bahari ya Hindi yatakuwa makubwa. Msimamo rasmi wa serikali ya Saudi Arabia hata hivyo haujulikani.

Uharamia ni tatizo kubwa. Kwa bahati nzuri kuna juhudi zinazochukuliwa na Italia na Ufaransa, kupambana na kitisho cha maharamia katika bahari ya Sham. Juhudi hizi zinapaswa kuungwa mkono na mataifa yote yanayopakana na bahari ya Sham. Uharamia unamuathiri kila mmoja. Kama vile ugaidi ulivyo kama ugonjwa, ambao tunapaswa kupambana nao.


Mwishoni mwa wiki iliyopita hata hivyo ghafla wamejitokeza wapiganaji wa Kiislamu kutaka kusaidia katika kuikoa meli hiyo ya Saudi Arabia. Tumewaweka wapiganaji wetu tayari, amesema msemaji wa kundi hilo la Waislamu kutokana na taarifa za kutekwa nyara meli hiyo zilizotolewa na shirika la habari la Reuters. Mkakati unaopangwa ni kuvunjilia mbali mawasiliano kati ya maharamia hao ndani ya meli na washirika wao ambao wako nchini Somalia. sababu kubwa ya kuchukuliwa hatua hiyo ghafla ni kutokana na kuwa meli hiyo inamilikiwa na kampuni ya Waislamu nchini Saudi Arabia. Kiini cha hali hii kinashangaza. Kwa kuwa nchi hiyo ya Kifalme kutokana na kuwa na uhusiano wa karibu na serikali ya Marekani , makundi mengi ya Kiislamu , ikiwa ni pamoja na Osama bin Laden mzaliwa wa Saudi Arabia, wanalazimika kupambana na taifa hilo linaloonekana kujitenga na Uislamu. Ni umbali gani mshikamano na Waislamu hao utafikia ni swali linalohitaji jibu. Duru nyingine zinadai , kuwa Waislamu hao huenda wakapata sehemu ya fedha zinazodaiwa na maharamia hao. Saudi Arabia haijasema lolote kuhusu pendekezo hilo la Waislamu wenye imani kali.

Waziri wa mambo ya kigeni anaweka wazi kuwa anaunga mkono hatua za kijeshi zinazoweza kuchukuliwa na jeshi la kimataifa.

Uharamia ni tatizo kubwa. Kwa bahati nzuri kuna juhudi zinazochukuliwa na Italia na Ufaransa, kupambana na kitisho cha maharamia katika bahari ya Sham. Juhudi hizi zinapaswa kuungwa mkono na mataifa yote yanayopakana na bahari ya Sham. Uharamia unamuathiri kila mmoja. Kama vile ugaidi ulivyo kama ugonjwa, ambao tunapaswa kupambana nao.



Alhamis iliyopita mataifa yanayopakana na bahari ya Sham yalifanya mkutano wao mjini Cairo ili kusaidia changamoto zinazokabili kwa pamoja mataifa hayo. Wamesisitiza kwa pamoja umuhimu wa kuheshimiwa eneo la maji la kila nchi. Suala ambalo limezushwa na Yemen, kutokana na kuwapo katika eneo lake kwa meli nyingi za mataifa ya kigeni ambazo zinapambana na maharamia wa Kisomali.


►◄