1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

jamii na kitisho cha itikadi kali

Grimmer/Oummilkheir10 Septemba 2007

Mapendekezo juu ya namna ya kukabiliana na wajerumani waliosilim

https://p.dw.com/p/CHRs

Wajerumani waliosilim,watabidi siku za mbele wawe wanapelelezwa.Biashara ya kemikali zinazoweza kutumiwa kutengeneza mabomu itabidi iwekewe vizuwizi na pabuniwe pia njia za kisheria zitakazohalalisha kunaswa mawasiliano ya kibinafsi ya Internet kama mkakati wa kupambana na ugaidi.Mapendekezo hayo ya wanasiasa baada ya kukamatwa watuhumiwa watatu wa kigaidi nchini Ujerumani,yamepokelewa kwa aina tofauti na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Tuanze lakini na STUTTGARTER ZEITUNG linaloandika:

„Jibu la wanasiasa kwa kitisho cha kigaidi si bayana na wala si la nguvu,panapohusika na shughuli za polisi , idara ya hifadhi ya katiba na idara ya upelelezi,katika kuendeleza uchunguzi wao dhidi ya watuhumiwa watatu waliotiwa mbaroni.Waziri wa sheria Brigitte Zypries anapendekeza biashara ya kemikali iwe inachunguzwa hivi sasa.Jambo hilo si baya,lakini halitasaidia chochote,kwasababu magaidi watabuni njia na mbinu nyengine za kujipatia vifaa wanavyohitaji.“

Gazeti la BERLINER ZEITUNG linaunga mkono fikra ya kupelelezwa wajerumani waliosilim.Gazeti linaendelea kuandika:

„Jamii haina njia nyengine isipokua kuwapeleleza waliosilim,ikiwa watu watataka kutofautisha kati ya wafuasi wa itikadi kali na wale wanaotumia nguvu.Na kwakua tokea hapo neno „tofauti“linatishia kutoweka,ingekua vyema kama watu wangejipeleleza wenyewe pia,mbali na kuwafanyia uchunguzi watu waliobadilisha dini.Hapo tuu ndipo uhuru wa kuabudu unapozaa uhuru wa mtu kujihami dhidi ya itikadi kali za kiislam.“

„Gazeti la WESTDEUTSCHE ZEITUNG la mjini Düsseldorf lina maoni tofauti na hayo na linaandika“:

„Mjadala kuhusu wajerumani waliosilim na kugeuka magaidi hauna kichwa wala miguu.Kwanza mwanasiasa wa Bavaria anaetazamiwa kua waziri mkuu,Beckstein,alipendekeza wajerumani wote waliosilim wachunguzwe.Hivi sasa tena katibu mkuu wa chama cha Christian Democratic CDU Ronald Pofalla amekuja na pendekezo jipya ili kushadidia imani ya dini ya kikristo:anataka misalaba ianze upya kutundikwa katika shule za serikali.Pendekezo la kwanza linamaanisha,yeyote anaejiambatanisha na dini ya kiislam anaweza kudhaniwa kua mwanaharakati wa Jihad.

Unaposikia tuu hoja kama hizo ,unatambua moja kwa moja,haziambatani na kifungu cha sheria msingi kinachohusiana na uhuru wa mtu kuabudu.Tungepaza sauti pia kama kwa mfano mturuki aliyebadilisha dini na kua mkiristo, angekabiliwa na dhana kama hizo?.Vipi watu waliosoma wanaweza kuzusha mjadala wa kipuuzi kama huu?“

Gazeti la MAIN –POST la mjini Würzburg linawasihi watu wawe na busara.

“Serikali na wanasiasa wana jukumu la kuwalinda raia dhidi ya mashambulio.Kwa uangalifu,bila ya kuutia dowa uhuru wa kila raia na bila ya tamaa ya kujipendekeza mtu au chama kwa lengo la kujipatia umaarufu.Ikiwa jamii ya magharibi itataka kujikinga kufika hadi ya kuuwekea vizingiti mtindo huria wa maisha,watakaofaidika hapo hawatakua wengine isipokua wale wale wapinzani wa mfumo wa kidemokrasi.”