1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yawahifadhi washukiwa wa mauaji ya Rwanda

7 Desemba 2010

Washukiwa wengi wa mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994 wanajificha nchini Kenya na Zimbabwe

https://p.dw.com/p/QRmD
Nembo ya mahakama ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Rwanda, ICTRPicha: UN

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya Umoja wa mataifa kuhusu Rwanda,ICTR, amesema Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inawahifadhi Wanyarwanda wengi waliohusishwa na mauaji ya kimbari 1994. Baadhi yao wanaaminika kuwa wanajificha Kenya na Zimbabwe. Mwendesha mashtaka Hassan Buabacar Jallow aliliarifu baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwamba kiasi ya watuhumiwa 10 wamebainika wanajificha nchini Kongo na serikali ya nchi hiyo imeahidi kushirikiana na mahakama kuhakikisha wanakamatwa.

Kulingana na takwimu, kiasi ya Wanyarwanda laki nane wengi wao Watutsi waliuwawa kati ya Aprili na Julai mwaka 1994. Bwana Jallow alisema kamanda wa zamani wa kikosi cha ulinzi wa rais wakati huo, Protois Mpiranya pamoja na mmoja ya watuhumiwa walioshtakiwa wanasemekana wanaishi Zimbabwe.