1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Ndege ya Indonesia imeshika moto wakati wa kutua

7 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLZ

Nchini Indonesia,ndege ya abiria ya shirika la Garuda imeshika moto wakati wa kutua kwenye uwanja wa ndege mjini Yogyakarta.Hadi watu 20 wamafariki baada ya kunasa ndani ya ndege hiyo.Kwa mujibu wa maafisa wa uwanja wa ndege,ndege hiyo ilishindwa kusimama ilipotua uwanjani.Waziri wa usafiri wa Indonesia,Hatta Rajasa amesema,abiria wapatao 93 wamenusurika. Ripoti zinasema,zaidi ya watu 130 walikuwemo ndani ya ndege hiyo iliyotokea mji mkuu Jakarta. Miongoni mwa abiria hao ni wanadiplomasia wa Australia na waandishi wa habari.