JAKARTA: Manusura 15 wa ajali ya feri waokolewa | Habari za Ulimwengu | DW | 08.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA: Manusura 15 wa ajali ya feri waokolewa

Manusura 15 wa ajali ya feri iliyotokea nchini Indonesia waliokolewa jana jioni baada ya kuelea majini kwa siku tisa. Afisa wa uokozi amesema mmoja wa manusura hao alifariki dunia muda mfupi baada ya kuokolewa na meli ya mizigo.

Operesheni ya kuwatafuta mamia ya manusura wengine wasiojulikana waliko mpaka sasa baada ya feri walimokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya kisiwa cha Java mnamo Disemba 29 mwaka jana, itapanuliwa.

Wakati haya yakiarifiwa, maofisa nchini Indonesia wanaendelea kuitafuta ndege ya abiria iliyopotea kufuatia hali mbaya ya hewa wiki moja iliyopita. Juhudi za kuitafuta ndege hiyo zinafanyika kisiwani Sulawesi na maeneo ya pwani ya kisiwa hicho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com