JAKARTA: Mafuriko yasababisha maafa Indonesia. | Habari za Ulimwengu | DW | 04.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA: Mafuriko yasababisha maafa Indonesia.

Watu kiasi tisa wamefariki na wengine takriban laki mbili wakaachwa bila makao baada ya mafuriko kutokea mjini Jakarta, Indonesia.

Maafisa wa serikali wanasema hayo ndio mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo tangu miaka mitano iliyopita.

Kwenye baadhi ya maeneo ya mji huo kina cha maji kimefikia urefu wa mita nne.

Maafisa wa utabiri wa hali ya hewa wametahadharisha huenda mvua kubwa ikazidi kunyesha mjini humo wiki ijayo.

Wafanyikazi wa shirika la msalaba mwekundu, pamoja na wafanyikazi wengine wa kujitolea wamekuwa wakigawa chakula kwa maelfu ya watu walioachwa bila makao.

Mafuriko hayo yamesababisha huduma ya nguvu za umeme kukatizwa na pia yamevuruga usafiri wa umma.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com