1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Kivuko kimezama pamoja na wachunguzi na wapiga picha

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOb

Nchini Indonesia,kivuko kilichoshika moto juma lililopita,kimezama kwa ghafula nje ya pwani ya Jakarta.Tume ya wachunguzi na wapiga picha walikuwemo katika chombo hicho.Mpiga picha mmoja amefariki na watu watatu hawajulikani walipo.Siku ya Alkhamisi kivuko hicho kilishika moto kilipokuwa njiani kuelekea kisiwa cha Bangka,nje ya Sumatra.Abiria walichupa baharini ili kujiepusha na moto.Si chini ya watu 41 wamepoteza maisha yao na kama 120 wengine bado hawajulikani walipo.