JAKARTA: Juhudi za uokoaji zaendelea kuwatafuta waathiriwa wa mkasa wa feri. | Habari za Ulimwengu | DW | 01.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA: Juhudi za uokoaji zaendelea kuwatafuta waathiriwa wa mkasa wa feri.

Kikosi cha wanamaji cha Indonesia kimeongeza juhudi zake kuwatafuta watu walioathirwa na mkasa wa feri uliotokea siku ya Ijumaa katika pwani ya Java.

Manusura walikaa baharini kwa usiku wa tatu kutokana na juhudi za uokoaji kutatizwa na hali mbaya ya hewa.

Mamia ya watu wamearifiwa kutoweka baada ya wavuvi na makundi ya uokoaji kufanikiwa kupata watu mia mbili miongoni mwa watu zaidi ya mia sita waliokuwa katika feri hiyo.

Maiti zaidi ya sitini zimeopolewa.

Feri hiyo iliyozama siku ya Ijumaa usiku, ilikuwa safarini kutoka kisiwa cha Borneo ikielekea bandari ya Semarang, Java

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com