1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

J3 0809 News

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRk

Freetown. Uchaguzi wa duru ya pili unafanyika leo.

Wapigakura nchini Sierra Leone wanapiga kura leo katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais. Kiongozi wa upinzani Ernest Bai Koroma anapambana na makamu wa rais Solomon Berewa wa chama tawala.

Katika uchaguzi wa duru ya kwanza uliofanyika kiasi cha mwezi mmoja uliopita, wagombea wote wawili hawakuweza kupata wingi unaohitajika wa asilimia 55 kuweza kushinda.

Koroma alipata asilimia 44 ya kura , ikilinganishwa na asilimia 38 alizopata Berewa. Ushindi wa wingi wa kawaida katika duru ya pili unahitajika ili kumpata mshindi.

Rais Ahmed Tejan Kabbah amezuiwa na sheria kugombea kwa awamu ya tatu.