1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

J2 2807 PRESSESCHAU

Kitojo, Sekione29 Julai 2008

Magazeti yamezungumzia kuhusu ziara ya Obama katika bara la Ulaya na mashariki ya kati, ongezeko la mafao kwa ajili ya watoto, na sera za ufufuaji uchumi nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/ElCU
Waziri wa uchumi wa Ujerumani Michael Glos(CSU) akizungumza na waandishi wa habari mjini Bonn hivi karibuni.Picha: picture-alliance / dpa


Ni wakati mwingine mpendwa msikilizaji wa kuyasikia maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani. Leo hii wahariri wengi wamezungumzia kuhusu ziara iliyomalizika mwishoni mwa juma ya mgombea wa kiti cha urais nchini Marekani Barack Obama katika bara la Ulaya, mpango wa ufufuaji wa uchumi nchini Ujerumani na haja ya kuongeza fedha kwa ajili ya watoto. Aliyewakusanyia maoni hayo leo hii ni Sekione Kitojo.


Tunaanza na gazeti la Badische Neueste Nachrichten la Karlsruhe ambalo linazungumzia ziara ya Barack Obama.


Gazeti linasema ni ugumu kiasi gani uliopo wa kuitekeleza sera ya kutokuwa na mizozo, na ni kiasi gani upo ugumu wa kuifanya diplomasia ifanyekazi , hilo linabaki wazi katika hali ya sasa ya shauku kubwa kumuelekea Obama. Anawezaje Ahmedinejad kuzipokea siasa hizi za ujenzi wa daraja? Iraq itaelekea wapi baada ya kuondolewa majeshi ya kigeni haraka iwezekanavyo. Obama hapaswi kujibu maswali haya. Inatosha , yeye kuwa mfano wa kuvutia na muokozi.


Gazeti la Der neue Tag, pia nae anazungumzia kuhusu Afghanistan na Obama.


Sasa amekuja Barack Obama linasema gazeti hilo na kushangiliwa na watu zaidi ya 200,000, akija na hesabu zake zisizoeleweka. Wanajeshi zaidi kwa ajili ya jeshi la NATO kwa maana hiyo anataka pia wanajeshi zaidi wa Ujerumani kwenda Afghanistan ili kusaidia kupunguza mzigo kwa walipakodi wake ambao ndio watakaompa kura. Mgombea huyo wa kiti cha urais anaunga mkono kwa hiyo, kile ambacho washirika wanakifikiria. Yeyote atakayekuwa rais , gazeti linadokeza, kutokana na ishara hii, kuna matumaini makubwa kwamba itawezekana kufanyakazi na Washington.



Kuhusiana na mpango wa kufufua uchumi nchini Ujerumani gazeti la Financial Times Deutschland, linalochapishwa mjini Hamburg linaandika:



Mpango huo wa waziri wa fedha, ni kitu kinachofahamika zamani , kama vile kurejeshwa kwa mafao ya watu wanaosafiri masafa marefu kwenda kazini na mafao ambayo hayapaswi kutozwa kodi, hali inayoonyesha hatari ya kuporomoka. Na wakati kansela mwanzoni mwa mwaka ujao atakapoleta dawa yake kuhusu suala hili, inawezekana kuwa tumechelewa kwa mpango huu wa ufufuaji wa uchumi.



Nalo gazeti la Offenbach-Post likizungumzia mpango huo linasema:



Tumwache waziri wa fedha Michael Glos kuukamilisha mpango huu wa ufufuaji wa uchumi. Ambao unaonekana kujumuisha hususan, vipengee, vya madai ya chama cha CSU kuhusiana na kampeni yake ya uchaguzi katika jimbo la Bavaria, ama pia uwezo wa kukubalika kwa vipengee vya huduma katika bajeti ya serikali, ambayo tayari ni sera ya serikali.




Kuhusu haja ya kuongeza fedha kwa ajili ya watoto gazeti la Münchner Merkur linasema:




Fedha kwa ajili ya watoto ni lazima ziongezwe. Lakini ni kiasi gani na kwa nani, kwa hilo serikali ya muungano haijakuwa pamoja. Kuhusiana na suala hilo kuna mapambano ya nadharia, utaratibu wa kifedha pamoja na matakwa maalum ambayo yanatofautiana.

Ili kupambana na hali ya umasikini, ni lazima watoto waondolewe kutoka katika hali ya kutengwa. Na wanahitaji vishawishi ambavyo wazazi wao hawawezi kuwapa.



Nalo gazeti la Kieler Nachrichten pia linazungumzia suala hilo la ongezeko la mafao ya fedha kwa ajili ya watoto. Gazeti linaandika.



Mahakama ya katiba katika mwaka 1999 iliamua kuwa kiwango cha chini cha mahitaji kwa watoto kisitozwe kodi na kwamba gharama za maisha ziangaliwe upya kila baada ya miaka miwili. Tangu wakati huo kwa bahati mbaya hakuna kilichotokea.



Kwa maoni hayo ndio tunakamilisha uchambuzi wa maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani kwa leo.



►◄