1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL:Uchaguzi mkuu wapendekezwa kufanyika 22 July

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5D

Kamati ya masuala ya kikatiba ya bunge nchini Uturuki imependekeza uchaguzi mkuu ufanyike july 22 badala ya juni 24 kama ilivyopendekezwa na waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan na chama chake cha AK.

Tarehe hiyo ya uchaguzi inatarajiwa kuidhinishwa na baraza kuu la bunge na kuondoa matumaini ya kumalizika haraka kwa mvutano kati ya wanaopendelea masuala ya dini katika serikali na wale wanaotaka dini itenganishwe na siasa.

Awali waziri mkuu Erdogan aliushutumu uamuzi wa mahakama wa kubatilisha uamuzi wa chama chake cha AK wa kumchagua Abdulla Gul kuwa mgombea wake wa Urais akisema ni kipigo kwa Demokrasia.

Siku ya jumanne mahakama ya kikatiba nchini humo ilifutilia mbali duru ya mwanzo iliyomchagua bwana Gul kugombea Urais baada ya upinzani kususia kura hiyo.