1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL:Gul ashindwa kupata kura nyingi za kumfanya awe rais

21 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXB

Mgombea urais kwa tiketi ya chama tawala nchini Uturuki cha AKP Abdulllah Gul ameshindwa kupata theluthi mbili ya kura katika bunge la nchi hiyo kumuwezesha kushinda kiti hicho.

Hata hivyo Gul ambaye ni waziri wa mambo ya Nje wa Uturuki na mwenye kuegemea zaidi itikadi za kidini anatarajiwa kushinda katika raundi ya pili ya uchaguzi wiki ijayo.

Uteuzi wake wa kuwania nafasi hiyo umepambana na upinzani kutoka kwa wale wasiyokuwa na mrengo wa kidini, wakiwemo makamanda wakuu wa jeshi na viongozi wa upinzani.

Kwa upande wake Gul ameahidi kuwa mwaminifu kwa katiba ya nchi hiyo isiyataka kuegemea katika itikadi za kidini.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelitaka jeshi la nchi hiyo kuwa mbali na siasa.

Hatua hiyo inafuatia wasi wasi kuwa iwapo Gul atashinda jeshi litaingilia kati kwa hofu kuwa atachukua mrengo wa kidini.