1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Istanbul. Polisi wakamata mtuhumiwa wa ugaidi.

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79N

Polisi nchini Uturuki wamemkamata , mtu mmoja raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki anayetuhumiwa kuwapa vifaa vya milipuko kundi moja la Waislamu ambalo linadaiwa linapanga kushambulia maeneo ya Wamarekani nchini Ujerumani. Mtu huyo anaaminika kuwa amekimbilia nchini Uturuki baada ya wenzake watatu kukamatwa katika msako wa polisi nchini Ujerumani miezi miwili iliyopita. Polisi wamekuwa wakilifuatilia kundi hilo, ambalo lilitayarisha kiasi kikubwa cha milipuko , kwa muda wa miezi kadha kabla ya kuwakamata.