ISTANBUL: Maandamano yapinga ziara ya Baba Mtakatifu | Habari za Ulimwengu | DW | 26.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISTANBUL: Maandamano yapinga ziara ya Baba Mtakatifu

Waandamanaji kwa maelfu wamekusanyika Istanbul kupinga ziara ya Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 nchini Uturuki.Ziara hiyo imepangwa kufanywa tarehe 28 Novemba hadi Desemba mosi.Maandamano hayo yameandaliwa na chama cha kisiasa cha kiislamu cha Uturuki.Viongozi wa chama hicho wanasema,wamehamakishwa na matamshi yaliotolewa na Baba Mtakatifu mwezi wa Septemba ambayo kwa maoni yao,yanahusisha matumizi ya nguvu na Uislamu.Ziara ya Papa nchini Uturuki itakuwa ziara yake rasmi ya kwanza kupata kufanywa katika nchi iliyo na wakazi wengi wa Kiislamu.Wakati wa ziara hiyo,Baba Mtakatifu huenda akautembelea pia msikiti maarufu mjini Istanbul.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com