1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yatangaza tenda ya ujenzi wa nyumba Jerusalem Mashariki

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXEf

TEL AVIV.Serikali ya Israel imesema kuwa imefungua tenda kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya 300 mashariki mwa Jerusalem eneo ambalo limetajwa kuwa linaweza kuwa ni mji mkuu wa taifa la Palestina.

Palestina kwa upande wake imesema kuwa hatua hiyo itazikwaza juhudi za hivi karibuni za amani kufuatia mkutano wa wiki iliyopita juu ya Mashariki ya Kati uliyofanyika huko Marekani.

Hata hivyo Israel imesema kuwa mpango huo kamwe hautaadhiri ushiriki wake katika mpango wa amani unaofadhiliwa na Marekani.

Pande hizo mbili Israel na Palestina zilikubaliana katika mkutano huo, kuufanyia kazi mpango wa amani wa mwaka 2003.

Wakati huo huo Rrais George Bush ametangaza kuwa atatembelea Mashariki ya Kati mwezi ujayo, ikiwa ni katika juhudi za kutafuta amani kwenye eneo hilo.