1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yapanga opresheni kali ya kijeshi ukanda wa Gaza

1 Machi 2008

Opresheni hiyo huenda ikasababisha mauaji ya halaiki imeonya Israel

https://p.dw.com/p/DG8N

Israel inapanga kuanzisha opresheni nzito ya kijeshi dhidi ya Ukanda wa Gaza ili kulipiza kisasi juu ya mashambulio ya roketi yanayofanywa na wanamgambo wa kipalestina kutoka eneo hilo linalodhibitiwa na chama cha Hamas.

Naibu waziri wa Ulinzi wa Israel Matan Vilnai amesema kupitia redio ya kijeshi ya Israel kwamba mashambulio ya roketi kutoka Gaza yanayoendelea huenda yakachochea opresheni kali ya Israel itakayosababisha mauaji ya halaiki ndani ya ukanda wa Gaza.Katika siku kadhaa zilizopita mashambulio ya angani ya Israel yameua kiasi cha watu 33 wa Gaza.Hali ya wasiwasi imeongezeka kwenye neo hilo baada ya wanamgambo wakipalestina wanaoendesha shughuli zai kutoka Gaza kufyatua makombora katika mji wa Ashkelon nchini Israel,mji ambao uko kilomita 10 kutoka kaskazini mwa Gaza.Jumatano iliyopita mashambulio ya roketi yalisababisha kuuwawa kwa mwanafunzi mmoja wa Israel katika mji ulioko mpakani wa Sderot.