1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaonya dhidi ya mashambulio ya wapalestina

12 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D6YX
Waziri wa ulinzi wa Israel, Ehud Barak, ameonya kwamba Israel itafanya kila jitihada kuwazuia wanamgambo wa kipalestina wanaouvurumisha maroketi nchini Israel kutoka kusini mwa Ukanda wa Gaza. Akiwa katika ziara yake ya siku mbili nchini Uturuki, waziri Barak anatarajiwa kukutana na rais wa nchi hiyo Abdullah Gul na waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan pamoja na viongozi wa jeshi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Israel, mazungumzo hayo yatatuwama juu ya mpango wa nyuklia wa Iran, ambao Israel inaamini unanuiwa kutumiwa kutengeneza bomu la nyuklia, dai ambalo linapinwa vikali na Iran.