1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yakiri mipaka ya 1967 iwe msingi wa mazungumzo ya amani

2 Agosti 2011

Israel na Marekani wanajaribu kufufua mazungumzo ya amani kwa misingi ya mipaka ya kabla ya mwaka 1967,ikiwa wapalastina wataachilia mbali madai ya kutaka watambuliwe na Umoja wa mataifa kama taifa huru.

https://p.dw.com/p/129Sr
Waziri mkuu wa Israel (kati)akihutubia katika bunge la MarekaniPicha: dapd

Kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa Israel ambae hakutaka jina lake litajwe,tangu wiki kadhaa zilizopita juhudi zimekuwa zikiendeshwa kufufua utaratibu wa amani na kuruhusu yaanze upya mazungumzo ya ana kwa ana kati ya waisrael na wapalastina.

"Fikra ni kwamba wapalastina wanaachana na mpango wao wa upande mmoja katika Umoja wa mataifa na juhudi hizo zimelengwa kuandaa muongozo utakaoruhusu mazungumzo yaanze"amesema afisa huyo aliyesisitiza Washington ndiyo iliyobuni fikra hiyo inayoungwa mkono pia na pande nne zinazosaka amani ya Mashariki ya kati,yaani Marekani,Urusi,Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.

Muongozo wa mazungumzo unataja juu ya kuwepo mataifa mawili kwa jamii mbili na kwamba Israel itambuliwe kama taifa la jamii ya wayahudi."Israel haitorejea katika mipaka ya mwaka 1967 na mpaka mpya utakaojadiliwa utabidi uzingatie hali iliyojitokeza katika kipindi cha miaka 40 iliyopita-amesema afisa huyo wa ngazi ya juu akimaanisha maeneo ya wahamiaji wa kiyahudi katika ukingo wa magharibi na eneo la mashariki la Jerusalem ambayo Israel inapanga kuyadhibiti pindi makubaliano ya amani yatafikiwa.

Dossierbild Frieden Nahost Netanjahu Obama Abbas 2
Benjamin Netanyahu(kushoto) akipeana mkono na Mahmud Abbas walipokutana na rais wa Marekani Barack Obama september 22 2009 mjini New-YorkPicha: picture-alliance/dpa

Kwa mujibu wa gazeti la Jerusalem Post,waziri mkuu Benjamin Netanyahu ameiambia kamati ya bunge inayoshughulikia siasa ya nje na ulinzi kwamba juhudi zinaendelezwa pamoja na Washington kuandaa waraka utakaorahisisha kuanzishwa upya mazungumzo kati ya Israel na Palastina.

Netanyahu amekumbusha kwamba rais Barack Obama wa Marekani aliwahi kusema waisrael na wapalastina watabidi wazungumzie "kuhusu mpaka ambao sio ule uliokuwepo hadi June nne mwaka 1967.

"Ni kifungu cha maneno kinachojulikana na wote wale ambao tangu kizazi kimoja kilichopita wamekuwa wakijishughulisha na suala hili.Kinawaruhusu watu wazingatie mabadiliko yaliyotokea katika kipindi cha miaka 44 iliyopita ikiwa ni pamoja na idadi halisi ya wakaazi walioko na mahitaji ya kila upande-ameongeza kusema waziri mkuu Benjamin Netanyahu.

Kwa mujibu wa Radio Israel Benjamin Netanyahu alishauriana kwanza na mkuu wa baraza la usalama wa taifa Yaakov Amidror kabla ya kuamua kuunga mkono pendekezo lililotolewa na rais Barak Obama May 19 mwaka huu kama msingi wa majadiliano.

Kontrollposten Grenzpolizisten nehmen Palästinenser fest Jerusalem Israel Flash-Galerie
Polisi wa Israel wanamkamata kijana wa kipalastina Jerusalem ya MasharikiPicha: picture-alliance/dpa

Mkuu wa ujumbe wa Palastina katika mazungumzo ya amani Saeb Erakat amemtolea mwito waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu "awaarifu walimwengu na vyombo vya habari kuhusu uamuzi wake wa kukubali mipaka ya amwaka 1967 ndio muongozo wa mazungumzo na kwamba atasaitisha kabisa ujenzi wa makaazi mepya ya wahamiaji wa kiyahudi katika ardhi za wapalastina ikiwa ni pamoja na Jerusalem ya Mashariki.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/afp,Reuters

Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed