1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel 'yaiziba' Gaza

18 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CtMD

GAZA:

Israel imeamuru kufungwa kwa njia zote za kuvukia kati ya Israel na eneo la Gaza.Hali itabaki hivyo kwa siku kadhaa na itaaathiri usafiri wa kibiashara pamoja na ule wa watu wa kawaida.

Tangazo hilo limekuja baada ya kuuliwa kwa waPalestina wengine watano katika shambulizi la Israel katika ukanda wa Gaza. Vifo hivyo vinajumulisha watu 29 kuwa wameuliwa tangu jumanne.Waziri mkuu wa Israel- Ehud Olmert -amesikitikia vifo vya watu wasio na hatia katika mashambulizi hayo.Hata hivyo ameapa kuendelea na hujuma dhidi ya wapiganaji katika eneo la Gaza,lengo likiwa kuzuia uvurumishwaji wa maroketi kwa Israel.