1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Uchaguzi mkuu Pakistan tarehe 6 Oktoba

20 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOH

Tume ya uchaguzi nchini Pakistan imetangaza tarehe sita mwezi ujayo kuwa ni siku utakaofanyika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Msemaji wa tume hiyo Muhammad Dilshad amesema kuwa siku ya mwisho ya kujaza fomu kwa wagombea ni tarehe 27 mwezi huu.

Rais Pervez Musharraf ametangaza kuwa atang´atuka katika cheo cha ukuu wa majeshi iwapo atashinda kipindi kingine cha pili cha uongozi.