ISLAMABAD:Muda wa rais Musharraf kumalizika mwezi Novemba | Habari za Ulimwengu | DW | 06.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Muda wa rais Musharraf kumalizika mwezi Novemba

Muda wa kuwa rais wa kiongozi wa kijeshi wa Pakistan jenerali Pervez Musharraf unamalizika tarehe 15 mwezi Novemba mwaka huu.

Kwa mujibu wa agizo la mahakama mawakili wa rais Musharraf wamesema kwamba kiongozi huyo anahitajika kueleza mipango yake ya uchaguzi.

Rais Musharraf mshirika wa karibu wa Marekani anapanga kutetea kiti chake cha urais kwa muhula wa pili wa kipindi cha miaka mitano licha ya kukabiliwa na shutuma kwamba anataka kujiongezea muda na kuendelea kuwa mkuu wa majeshi wa Pakistan.

Jaji wa mahakama kuu Iftikhar Muhammad Chaudhry ametoa agizo kwa serikali itangaze tarehe maalum ya rais Musharraf atakapokamaliza muhula wake kwenye ofisi ya rais.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com