1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Mpiganaji wa Taleban ajilipua kwa guruneti

Mpiganaji mmoja wa ngazi za juu wa Kundi la Taleban nchini Pakistan amejilipua wakati wa mapigano na majeshi ya usalama.Abdullah Mehsud anayesakwa kwa madai ya kuwateka wahandishi wawili raia wa Uchina mwaka 2004,alijilipua kwa guruneti.Majeshi ya usalama yalivamia maficho yake jana usiku katika wilaya ya Zhob kusini mwa mkoa wa Baluchistan.

Wakati huohuo jeshi la Pakistan linathibitisha kuwa limewaua yapata wapiganaji 35 katika eneo la Waziristan ya Kaskazini linalopakana na Afghanistan.Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Pakistan waanjeshi 12 walijeruhiwa katika mapigano mapya yaliyoanza jumapili usiku.Wapiganaji hao walitumia makombora ya roketi na zana nzito katika mapigano hayo yaliyodumu kwa saa kadhaa.

Hali ya wasiwasi imetanda kwenye eneo hilo tangu wiki jana wakati wapiganaji wanaounga mkono kundi la Taleban walitangaza kujiondoa kwenye makubaliano ya amani yaliyofikiwa na serikali mwaka 2006.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com